300x250 AD TOP

Powered by Blogger.

Life & style

Popular Posts

Marafiki Waliotembelea Blog

Technology

NGOMA

Featured Video

UDAKU

Recent Posts

Popular Posts

May 9, 2013

Tagged under:

Soka-BARCELONA KUSUBIRI MPAKA JUMAPILI ILI KUWA MABINGWA WAPYA WA LA LIGA

Kutokana na ushindi bao 6-2 wa Real madrid dhidi ya Malaga nyumbani Santiago Bernabeu jana jumatano kumeifanya Barcelona ambao ni vinara wa ligi kuu nchini hispania maarufu kama La Liga kusubiri mechi yao ya jumapili dhidi ya Atletico Madrid itakayopigwa katika dimba la Vicente Calderon.

Barca inahitaji point 2 tu katika mechi zao 4 zilizosalia kutawazwa kuwa mabingwa mara 22 wa taji la ligi kuu nchini humo.Huu utakuwa muendelezo wa mabingwa katika ligi kubwa barani ulaya kutwaa ubingwa huku wakiwa na mechi mkononi.Barca iliyo mbele ya Madrid kwa tofaiti ya pointi 8 tu huku wapinzani wao Madrid wakiwa wamecheza idadi kubwa ya mechi kuliko Barcelona inayohitaji kushinda mechi yake ya jumapili ili kutengeneza tofauti ya pointi 11 kati yake na Madrid na kujitangaza mabingwa kwani kwa tofauti hiyo hakuna timu yoyote itakayoweza kufikia pointi ambazo Barca watakuwa wamezifikisha.

Utakuwa ni ubingwa wa 4 kwa Barca katika miaka mitano ya mafanikio ambayo yatakua yanaenda sambamba na jina lao walilopewa "THE DREAM TEAM".Pia Atletico itakuwa inaangalia mchezo wa fainali wa kombe la mfalme [COPA DEL REY] dhidi ya Real Madrid wiki chache zijazo lakini kocha wa Atletico Diego Simeone amesema yeye na wachezaji wake hawatatishwa na uwezekano wa majirani zao Real kumaliza msimu bila kupata medali yoyote kubwa msimu huu.
"Hatutaruhusu uwezekano wa sisi kupoteza mchezo huo kwa kuwa hatutaongeza vitu tofauti katika mchezo huo,tunahitaji kufikiria zaidi mchezo wetu dhidi ya Barca"Simeone aliyasema hayo alipokua anazungumza na mkutano wa waandishi wa habari hapo jana jumatano.

"Tunajua utakuwa mchezo mgumu hiyo jumapili lakini mashabiki watakuwa na sisi kutushangilia kitendo ambacho kitatufanya tuweze kufuzu ligi ya mabingwa wa ulaya [UEFA].Itakua ni changamoto kwetu na tutaona hiyo kesho ni vipi wachezaji wanaufikiria huu mchezo".Aliongeza muargentina huyo.

0 your comments:

Post a Comment