Kigali, Rwanda
Jeshi la Rwanda limeiokosoa Marekani baada ya
kuiwekea vikwazo kwa madai kwamba limekuwa likiwasaidia wapiganaji wa
Kundi la M23.
Taarifa zilisema kuwa Marekani ilichukua uamuzi
huo baada ya kulituhumu Jeshi la Rwanda kwamba liliwasaidia wapiganaji
wa M23 waliopo Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC)
kuwatumikisha watoto jeshini.
Msemaji wa Jeshi la Rwanda, Joseph Nzabamwita
alisema kuwa tuhuma hizo za Washington hazina ukweli na wala hazina
ushahidi wowote.
Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Marekani
ilitangaza kuwa nchi hiyo ilisimamisha misaada ya kifedha na kijeshi kwa
nchi hiyo kwa mwaka wa fedha wa 2014.
Wakati huohuo, ujumbe wa
wataalamu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ulielekea katika eneo
la Ukanda wa Maziwa Makuu ya Afrika kwa shabaha ya kutoa msukumo wa
usalama na amani katika eneo hilo.
Taarifa ya Umoja wa Mataifa ilieleza kuwa, ujumbe
huo utakutana na marais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Rwanda,
Uganda na Waziri Mkuu wa Ethiopia.
Umoja wa Mataifa unaituhumu Rwanda kwa kuwaunga
mkono M23 katika harakati zao dhidi ya Serikali ya Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo madai ambayo Rwanda imekana.
Kundi la M23 lilianzishwa na waliokuwa waasi wa Kitutsi waliojiunga na Jeshi la DRC chini ya mkataba wa amani wa mwaka 2009
Mwaka 2012 mwezi Aprili waasi hao wa M23
waliwageuka waliokuwa wanajeshi wenza na kuanza uasi Mashariki mwa nchi
ambako kuna utajiri mkubwa wa madini.
SOURCE:
Mwananchi
SOURCE:
Mwananchi
0 your comments:
Post a Comment