300x250 AD TOP

Powered by Blogger.

Life & style

Popular Posts

Marafiki Waliotembelea Blog

Technology

NGOMA

Featured Video

UDAKU

Recent Posts

Popular Posts

Oct 21, 2013

Tagged under: ,

Michezo| Manji, Hanspope waonyeshana ubabe Uwanja wa Taifa.


MATAJIRI wawili wenye hamasa kubwa kwa mashabiki wa Simba na Yanga, Zacharia Hanspoppe (Simba) na Yusuph Manji (Yanga) jana Jumapili walionyesha ubabe kwa muda kwa kucheza na akili za mashabiki wao kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Tukio hilo lilitokea wakati wa kuanza kwa mchezo, mapumziko na dakika za mwisho lakini kishabiki Hanspoppe alionekana kumzidi kete Manji kwavile timu yake ilimkomboa kwa kuchomoa mabao na kulazimisha sare ya mabao 3-3.
Wakati mpira unaanza Manji ambaye ni Mwenyekiti wa Yanga aliingia uwanjani hapo akiambatana na makamu wake, Clement Sanga na kabla hawajakaa, Manji alizunguka akihamasisha mashabiki kuhesabu vidole vitano akimaanisha Yanga ingeshinda kwa mabao matano kitendo ambacho kilishangiliwa na mashabiki wa Yanga.
Hanspoppe ambaye ni Mwenyekiti wa Usajili wa Simba, alipoona hivyo alisimama na kuwahamasisha mashabiki wa Simba na kuwaonyesha ishara ya mabao matatu na kuwaambia watulie.
Hata hivyo hadi mapumziko Yanga walikuwa wanaongoza kwa mabao 3-0 jambo ambalo lilimpa kiburi Manji na wakati wa mapumziko akahamasisha tena mashabiki wake akimaanisha goli zilezile tano.
Lakini upepo ukambadilikia kipindi cha pili timu yake iliporuhusu mabao yote matatu yakarudi ndipo Hanspoppe akainuka na kuanza kutamba tena huku Manji na Yanga wote wakanywea kwa kutoamini kilichotokea.
Mpaka mchezo unamalizika Yanga walikuwa wamenywea huku Simba wakiongozwa na Hanspoppe walikuwa wakishangilia sare hiyo ambayo ni kama ushindi kwa vile walichomoa bao zote na kuwaacha Yanga midomo wazi.
Baada ya mchezo huo Yanga walinywea mitaani huku Simba wakizunguka wakipiga kelele kwa mbwembwe nyingi kama wametwaa ubingwa.
Jijini la Dar es Salaam lilikuwa limezizima kwa kelele za mashabiki wa Simba ambao walikuwa wakishangilia kwa kutumia honi za magari, mavuvuzela na maneno ya kebehi.

Source:Mwanaspot

0 your comments:

Post a Comment