KIUNGO wa Schalke 04, Kevin-Prince Boateng na mdogo wake, Jerome Boateng anayekipiga Bayern Munich wanachekesha sana. Ni ndugu wa baba mmoja, lakini wanatoka matumbo tofauti.
Kama hiyo haitoshi, makuzi yao ya mahangaiko jijini Berlin yamewafanya wawe na bifu za kitoto pia.
Amnyima tiketi mdogo wake
Wiki iliyopita, Bayern Munich ilisafiri mpaka
Schalke kukipiga na Schalke 04 katika pambano la Ligi Kuu Ujerumani.
Pambano hilo lilipigwa katika Uwanja wa Gelsenkirchen.
Kabla ya mechi, Jerome alimuomba tiketi ya bure
kaka yake kwa ajili ya kumpatia rafiki yake au mpenzi wake. Hata hivyo
saa chache kabla ya mechi, Kevin alimtumia mdogo wake ujumbe katika simu
uliosomeka: “Siwezi kukupatia tiketi yoyote. Samahani.”
Jerome alifichua siri hiyo wakati akizungumza na
waandishi wa habari huku akikiri kwamba ni wazi kwamba kaka yake alikuwa
amemnyima tiketi. Si tiketi tu, Kevin ana chumba chake maalumu cha
kutazamia mechi uwanjani Gelsenkirchen katika eneo la watu maalumu,
lakini alikuwa ameamua tu kumfanyia roho mbaya mdogo wake.
Wakati wa mapumziko wa pambano hilo, wawili hao
walikumbatiana kwa furaha na kubadilishana jezi, huku wakiongea maneno
mawili matatu.
Baba yao ataka wakasirikiane
Baba yao anayejulikana kwa jina la Prince Boateng
aliondoka nchini Ghana mwaka 1981 kwenda Ujerumani kwa ajili ya kusoma
masomo ya Utawala.
Hata hivyo masomo yalimshinda na badala yake akaingia katika kazi ya muziki akiwa DJ na vile vile akiwa mhudumu wa baa.
Kevin-Prince alikuwa na umri wa miaka miwili
wakati baba huyo alipoiacha familia nyumbani na kusababisha mama yake wa
Kijerumani atumie muda mwingi kuwalea yeye na mdogo wake, Jerome ingawa
mama wa Jerome ni mwingine.
SOURCE
Mwanasport
SOURCE
Mwanasport
0 your comments:
Post a Comment