Inafahamika kwa jina la Aeromobil version 2.5, gari ambayo imegunduliwa na mmoja kati ya wanasayansi ambaye pia ni Engineer wa Kislovakia Stefan Klein,historia yake inamjumuisha kwenye utengenezaji wa Gari tofautitofauti ikiwemo Audi na BMW.Inaelezwa gari hili linatumia Injini moja ya Ndege inayokwenda kwa jina la 100-hp Rotax ambayo inauwezo wa kupiga masafa ya barabarani takribani Maili 310 kwa mafuta na Maili 430 angani kwa mafuta maalum yanayoweza kuendesha Injini hiyo yenye mchanganyiko wa Aina mbili za injini.
Klein anasema alipata wazo la kuitengeneza gari hiyo takribani miongo miwili iliyopita mpaka kufanikisha hilo,na kuongeza kuwa anategemea Aeromobil Version 3.0 iko tayari kutokana na kukamilisha Aeromobil Version 2.5.Mwanasayansi huyo bado yuko kwenye hatua za mwisho za kuweza kuikamilisha akiongeza kwa kusema "changamoto kadhaa bado nazifanyia kazi ikiwemo pale ambapo gari hiyo ilipopaa mbali zaidi kushuka kwake kulikuwa na mapungufu zaidi hapo awali wakati inajaribiwa"
SWALI:kama mwanasayansi huyu wa Kislovakia anatumia zaidi ya Miongo miwili akifanya uchunguzi wa kitu,jeee!!kwa wanasayansi wa Kitanzania hawawezi kufanya hivyo ili kufanya kitu kama cha Klein?!!
0 your comments:
Post a Comment