Masanja Mkandamizaji si jina geni masikioni mwa watu wengi
kutokana na uwezo wake wa kuwavunja mbavu watazamaji pale anapoonekana
katika runinga na Kundi la Original Comedy.
Licha ya kufika hapo alipo sasa, anakiri wazi kuwa amepitia
katika maisha magumu hususani wakati alipoamua kuanza maisha binafsi ya
kujitegemea baada ya kutoka nyumbani kwa dada yake alipokuwa akiishi.
Anasema kabla ya kuondoka kwa dada yake alimuomba amtafutie
chumba ili ajitegemea na kuanza maisha binafsi kama kijana . Nilimwambia
dada anitafutie chumba na alifanya hivyo ingawa alikuwa anahofia kama
nitaweza ,basi nikapata 'geto' langu maeneo ya Tabata Aroma na
nilitakiwa kulipa kodi ya TSh. 5,000 kwa mwezi, anasema Masanja. Anakiri
wazi kuwa changamoto katika maisha ndizo zilizochangia kumfikisha
mahali alipo sasa kwani licha ya kuwa katika hali ngumu
Hakukata tamaa bali alizidi kujituma kwa nguvu zake zote.
Anasema kuna wakati ilikuwa vigumu kuipata hata hiyo hela ya kodi
kwahiyo ilikuwa inamlazimu kurudi kwa dada yake kwa muda unapofikia
wakati kulipa kodi. Yaani hiyo TSh. 5,000 kuipata ilikuwa shughuli maana
ilikuwa ikifika karibu na mwisho wa mwezi narudi kwa dada kuzuga kidogo
ili mama mwenye nyumba ajue nimesafiri,anasema. Anasema alianza kwa
kulala chini mpaka siku alipofanikiwa kupata fedha kidogo iliyomuwezesha
kununua godoro la sufi jambo ambalo anajivunia nalo kwani aliweza
kununua kwa jasho lake.
Anaongeza kuwa kamwe hawezi kumsahau marehemu Steven Kanumba
pamoja na mtu mwingine aliyemtaja aitwaye Mtitu kutokana na mchango wao
uliosaidizi kumfikisha hapo alipo sasa.
“Namshukuru sana marehemu Kanumba alikuwa anakuja kunichukua
kule Tabata tunaenda kupiga 'inshu' ambazo zilikuwa zikiniingizia pesa
kidogo iliyoniwezesha kuishi hata hivyo maisha yalikuwa magumu. Wakati
naanza maisha sikuwahi kutoa hela hata ya kununua chipsi kavu lakini
siku moja nilifanya kazi na Mtitu ambayo alinilipa laki moja sikuamini
macho yangu, kwa mara ya kwanza kununua chipsi kuku kwani nilikuwa
nikitamani mlo huo nililazimika kusaidia kumenya viazi kwa washikaji” alieleza Masanja.
Sambamba na uchekeshaji Masanja pia amejiingiza katika shughuli
za kumtukuza Mungu baaada ya kuokoa na sasa anafanya vizuri pia katika
uimbaji wa nyimbo za injili na kesho Jumapili atazindua albamu yake ya
pili ya muziki wa Injili inayoitwa Hakuna jipya chini ya jua.
By:BONGOMOVIE
Feb 15, 2014
Tagged under: Entertainment, News, Social
Historia| Fahamu maisha aliyopitia Masanja Mkandamizaji mpaka hapa alipo sasa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 your comments:
Post a Comment