Jimbo la Arizona nchini marekani
limeanzisha mchakato wa kuahalalisha Bangi iwe kilevi kama vilevi vingine
ikiwemo Pombe.
Mchakato huo ambao ulitangazwa
jumanne ya April 12 mwaka huu,kwa sasa upo
kwenye uchukuaji wa Saini za wakazi wapatao 201,158.
Kwa mujibu wa mtandao wa Kampeini
hiyo unatarajia kukusanya zaidi ya
Saini 201,158 ili kuruhusu zoezi kufanikiwa kwa kuwa baadhi ya
watakaoweka Saini hawatojitokeza kupiga kura ya kuipitisha sheria hiyo ifikapo
mwezi Novemba mwaka huu ambapo nusu ya kura zitakazopendekeza Bangi iwe Kilevi
sawa na vilevi vingine itaruhusiwa kisheria kutumiwa na watu walio zaidi ya
umri wa miaka 18.
Kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi kufikia
Juni mwaka huu jumla ya Saini 150,642 zinahitajika kutoka kwa watu
waliosajiliwa kushiriki chaguzi mbalimbali katika jimbo la Arizona ili kuona
ulinganifu wa zoezi la upigwaji kura Mwezi Novemba mwaka huu.
Kampeni hiyo ya kuihalalisha Bangi
iwe kilevi halali kama Vilevi vingine unaratibiwa na mpango maalum ambapo kwa
sheria za utumiaji Madawa ya kulevya katika jimbo hilo kodi asilimia 15 inatoka
katika upande wa Bangi japo haitumiki kihalali kwa matumizi ya kilevi lakini
kiwango kinachopatikana kutokana na kodi hiyo hupelekewa katika shughuli za
kijamii ikiwemo shule za serikali katika jimbo hilo.
Kwa mujibu wa Waratibu wa Kampeni ya
kuruhusu Bangi iwe sawa na Vilevi vingine wanadai huenda kampeni hiyo
isifanikiwe kulinagana na uzito wa sheria za Marekani unaobana Matumizi ya
Bangi kihalali japo yanatumiwa na Wamarekani.
Kusoma zaidi BOFYA HAPA
0 your comments:
Post a Comment