300x250 AD TOP

Powered by Blogger.

Life & style

Popular Posts

Marafiki Waliotembelea Blog

Technology

NGOMA

Featured Video

UDAKU

Recent Posts

Popular Posts

Nov 29, 2012

Tagged under:

BURUDANI:JUSTIN BIEBER AMEINGIA KWENYE LIST YA WASANII 10 BORA WA MWAKA WENYE PESA NYINGI.

Justin Bieber
          Ingawa ni ana umri wa miaka 18 tu,ila naweza sema huu ulikuwa mwaka wake katika mafanikio ya kimziki hapa namzungumzia bwana mdogo raia wa Canada Justin Bieber amabaye mpaka sasa amekwisha kuachia album yake ya tatu,kutnagaza ziara ya majira haya ya baridi,uwekezaji katika mambo mbalimbali ya kibiashara,na mengineyo,yote kwa yote ndani ya miezi 12 yaani mwaka mmoja ameweza kuingiza kitita cha fedha zaidi ya dollar za kimarekani million 55.          Akizungumza na mtandao wa FORBIES Bieber amesema 'kila wiki nimekuwa nikiwaita watu wangu yaani mwanasheria pamoja na mfanyabiashara wangu,kila wiki nimekuwa nikijifunza kitu kuhusu biashara zangu na jinsi gani nifanye katika kazi yangu(mziki).
        Lakini kwa upande mwingine Bieber ni msanii wa kidunia ambapo kwa mujibu wa mtandao wa FORBIES msanii huyu ameingia kwenye kumi bora ya wasanii waliojiingizia hela nyingi kutokana na kazi yao wanayoifanya.Akiwemo mkali wa HipHop Dr.Dre ambaye kupitia mpango wake wa usambazaji vifaa vyake vya kimziki ikiwemo headphone za Beats by Dre ambao ulimwingizia Dollar za Marekani zipatazo million110,'ukiangalia wanaoingiza pesa ndefu kupitia kazi zao huyu jamaa amekuwa akifanya vizuri tangu miaka 20 iliyopita mpaka leo jamaa anajua kipi anachokifanya', ni baadhi ya maneno ya aliyekuwa Rais wa Def Jam Recordings Kelvin Liles ambaye kwa sasa anasimamia kazi za Young Jeezy na Trey Songz.
Dr.Dre
Japo wapo pia akina Jay-Z pamoja naye P.Diddy ambao asilimia kubwa wamejikusanyia pesa nyingi kupitia ziara mbalimbali za kimziki.
Jay Z na mtu mzima P.Diddy
Kati ya wasanii walioingia katika list ya wasanii 10 bora ukiwatoa Justin Bieber,Dr.Dre,Jay-Z,P.Diddy wapo pia Pink Floyd rocker Rogers Water-$88millions,Elton John-$80millions,Adele-$72millions,British Boy Band $69millions,Taylor Swift-$57millions sawa na Paul McCartney.
Kundi la British Boy Band wakiwa katika moja ya uwajibikaji
Takwimu za kujua orodha ya mastaa hawa zimechukuliwa kwa makadirio tokea mwezi wa 5 mwaka 2011 hadi mwezi wa 5 mwaka 2012 na hii ikiangaliwa saana katika kazi za wasanii walizofanya zikawasababishia kuingiza fedha hizo ikiwemo mauzo ya kazi zao,mapato ya ziara zao,pamoja na shughuli mbalimbali ikiwemo uwekezaji wa kwao binafsi katika biashara,nakadhalika hii yote ni kabla ya kodi na makato mbalimbali kabla hayajafanyika,na mchakato huu uliwahusisha watu mbalimbali wanaojihusisha na masuala mbalimbali ya kijamii wakiwemo mapromota wa matamasha,wanasheria,mameneja,mawakala pamoja na wasanii wenyewe.


0 your comments:

Post a Comment