Justin Bieber akiwa na moja ya tuzo zake |
Usiku wa jumapili katika jiji la Los Angels kulifanyika event kubwa maarufu nchini Marekani nayo ni tuzo za mziki za Amerika almaarufu America Music Awards(AMAs2012) mwaka huu,huku msanii mwenye umri mdogo na anafanya vizuri kwa sasa tokea marekani Justin Bieber akiibuka na tunzo kubwa ya msanii bora wa mwaka,na hii imekuwa ni neema nyingine kwa star huyo mdogo kwani inazidi kumweka katika nafasi nzuri kwenye ramani ya mziki duniani.
hapa ni Nick Minaj akiwa kikaazi zaidi na bw.mdogo Justin Bieber |
Lakini pia aliweza kuchukua tuzo ya msanii bora wa kiume katika miondoko ya Pop/Rock(Favorite Pop/Rock Male Artist) na baada ya kuichukua tuzo hiyo aliweza kusema 'hii inaenda kwa wanaonichukia na wanaodhani niko kwenye game kwa mwaka mmoja au miwili,najisikia nitakuwepo kwa muda mrefu saana'
Katika tuzo yake hiyo ya pili Bieber alionekana akipita mbele ya jukwaa akiwa ameshikana mmkono na mamayake mzazi na kusema maneno maneno machache akimwongelea mama yake'She's little,but she's beautiful' akimaanisha kuwa nimdogo lakini ni mrembo.Baada ya pale Bieber aliweza kumshukuru mama yake akisema 'najiona kama niko mbali saana kwa sasa,ahsante mama kwa kuniamini.
ANGALIA HAPA BAADHI YA PICHA KWENYE TUZO ZA AMERIKA MAARUFU KAMA (AMAs2012) IKIWEMO AMAs2012 RED CARPET.
picha mbalimbali za AMAs2012 Red Carpet |
Justin Bieber na wengine katika AMAs2012 Red Carpet |
0 your comments:
Post a Comment