kushoto ni mgombea kwa tiketi ya chama cha ODM(Orange Democratic Movement) Raila Odinga,kulia ni Uhuru Kenyatta toka chama cha Nationa Alliance Party(NAT) |
Serikali ya Kenya imekanusha madai kuwa
kuna njama ya wizi wa kura katika uchaguzi mkuu ujao mwezi Machi 4 kwa
niaba ya Muungano wa Jubilee wake Uhuru Kenyatta.Msemaji wa serikali Muthi Kariuki alisema kuwa
madai yaliyotolewa na muungano wa CORD wake waziri mkuu Raila Odinga
hayana msingi na kuna hofu kuwa huenda madai hayo yakachochea hali ya
wasiwasi na taharuki miongoni mwa wafuasi wa pande hizo mbili.
Aliutaka Muungano wa Cord kutafuta sera za kuwauzia wakenya ili waweze kuwachagua badala ya kueneza propaganda na kutishia usalama wa nchi
Bwana Muriuki alisema kuwa mkuu wa utumishi wa Umma, Francis Kimemia alitoa onyo kwa wafanyakazi wa umma kuwaonya wafanyakazi wa umma dhidi ya kujihusisha na kampeini au maswala ya siasa.Madai ya CORD yamekuja wakati pande zote mbili zinarushiana madai ya njama ya wizi wa kura. Wiki iliyopita Jubilee au upande wa Uhuru Kenyatta ulidai kuwa pande CORD wana njama ya kuwalewesha wapiga kura wao usiku mkesha wa uchaguzi.
0 your comments:
Post a Comment