Kundi la wapiganaji la Ansaru, limedai liliwateka nyara wafanyakazi saba wa kigeni na kumuua mlinzi wakati wa tukio hilo.Wafanyakazi kutoka Italia, Ufilipino,
Uingereza, Ugiriki na Lebanon yasemekana ni kati ya wale waliotekwa
nyara katika jimbo la Bauchi Kaskazini mwa Nigeria.Wafanyakazi hao walikuwa kazini katika kiwanda kimoja wakati wapiganaji hao walipowateka nyara siku ya Jumapili.
Mapema leo, polisi nchini humo walianzisha msako dhidi ya watu waliowateka nyara wafanyakazi hao.
Mlinzi katika kampuni hiyo ya ujenzi, Septraco,
inayomilikiwa na watu wenye asili ya Lebanon, alipigwa risasi na kuuwawa
kwenye ua la kampuni hiyo.Septraco inapanua barabara moja kuu katika jimbo
la Bauchi. Awali, kituo cha polisi katika mji wa Jama'are
kilishambuliwa na magari mawili kulipuliwa.
Mapema mwezi huu, watoa chanjo za polio tisa walipigwa risasi na kuuwawa katika zahanati mbili hukuhuko kaskazini mwa Nigeria.Kudni la Ansaru ambalo lieanza harakati zake
mwezi Juni mwaka jana, iliwatumia wandishi wa habari barua pepe kusema
kuwa hao ndio waliohusika na kitendo hicho.
Wizara ya mambo ya nje ya Uingereza hata hivyo
ilikimya kuhusu ikiwa raia wa Uingereza alikuwa miongoni mwa wale
waliotekwa nyara.
Visa vya utekaji nyara ni jambo la kawaida nchini Nigeria hasa watu matajiri na wafanyakazi wa kigeni ndio walengwa sana.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 your comments:
Post a Comment