Feb 13, 2013
Tagged under: Sport
Wapenda soka nchini wakiwemo wale waliotoka mikoani kuwenda Dar es Salaam ili kumwona nyota wa Cameroon, Samuel Eto'o Fils wakati timu yake ya taifa Indomitable Lions ilipomenyana kwenye mechi ya kirafiki na Taifa Stars Uwanja wa Taifa, Jumatano iliyopita matokeo yake hawakuweza kumwona mshambuliaji huyo anayekipiga kunako klabu ya Anzhi Makhachkala ya Urusi.
Timu yake ikalala bao 1-0 huku taarifa za awali kupitia benchi la ufundi la Cameroon likatoa ufafanuzi kwa Watanzania kwamba straika huyo alikuwa majeruhi. kitu ambacho hakikuwa sahihi.
Sasa yeye mwenyewe ameibuka na kutamka kuwa aligoma kuja nchini kutokana na kuhofia kuuawa.Nahodha huyo ameibua mjadala mzito baada ya kuwatuhumu maofisa wa Shirikisho la Soka la Cameroon (FECAFOOT) kwa kutaka kumuua.
Sambamba na kauli hiyo, Eto'o, amesema kwamba yuko tayari kwa mjadala wa suala hilo ambao utarushwa moja kwa moja kupitia televisheni ya taifa.Wanataka kuniua, katika timu ya taifa naishi na mashushushu, si kwamba siko makini katika hilo kwani hata jezi ya timu ya taifa navaa yangu binafsi niliyotengenezewa na Puma, alisema mchezaji huyo kupitia Jarida la Je Wanda la Cameroon.
Etoo ambaye kwa sasa anachezea klabu ya Anzhi Makhachkala ya Urusi pia alisema kwamba hata anapokuwa mazoezini wakati wote yuko makini na maisha yake.Etoo ni miongoni mwa wachezaji 11 wa Cameroon ambao hawakuitikia wito wa kuichezea timu hiyo mechi ya kirafiki dhidi ya Tanzania iliyopigwa Jumatano iliyopita na Cameroon kulala bao 1-0 lililofungwa na Mbwana Samatta.
Hawa wazee wametafuna fedha zetu kiasi cha kutosha, badala ya kusimamia soka kwa ajili ya umma wako katika mipango ya uongo, kusafiri daraja la kwanza kwenye ndege na kunufaisha akaunti zao za siri katika mabenki ya Ulaya, alisema.Cameroon itaumana na Togo mwezi ujao katika mechi ya awali ya fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2014 na Etoo anadhani timu hiyo haina uwezo wa kuifunga Togo.
Shirikisho la soka nchini Cameroon(FECAFOOT)hakijasema lolote kuhusu hoja hizo za Etoo ingawa mmoja wa maofisa wa shirikisho hilo anadaiwa kumwambia Etoo kuwa amekosa uzalendo na hoja zake ni kichekesho.Kocha wa Cameroon, Jean Paul Akono, alisema jijini Dar es Salaam kwamba anataka kupunguza wachezaji wenye umri na majina makubwa kwenye kikosi hicho na kutengeneza kizazi kipya kitakachorejesha heshima ya Taifa hilo kisoka.
Sports| Samuel Eto'o:Kumbe hakuja Tanzania na timu ya Cameroon akiogopa kupoteza uhai wake.

Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 your comments:
Post a Comment