MBUNGE wa Viti Maalumu wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema), Mwanamrisho Taratibu Abama jana asubuhi aliugua na kuanguka ghafla katika viwanja
vya Bunge na kukimbizwa hospitali.Tukio hilo lilitokea wakati akienda
kuhudhuria
semina ya wabunge kuhusu Rasimu ya Sera ya Gesi Asilia kabla ya kukosa
nguvu na kudondoka na kisha kusaidiwa na wenzake kumkimbiza kwenye
zahanati ya Bunge.
Baada ya kupatiwa huduma ya kwanza bungeni, gari la
wagonjwa lilimkimbiza Hospitali ya Mkoa wa Dodoma (General) ambako amelazwa.Kwa mujibu wa waliomshuhudia, mbunge huyo alianza kwa kuishiwa nguvu hali ambayo waliokuwa
karibu walimsaidia kumpeleka kwenye zahanati ambako alitundikiwa
dripu ya maji kabla ya kupelekwa hospitalini.Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Dodoma, Zainabu Chaula alikiri kumpokea mbunge huyo.
0 your comments:
Post a Comment