Rehema Shauri Madongo ni mmoja kati ya mwanamke ambaye amebahatika kuolewa na askari polisi kitendo cha upelelezi ambaye anaeleza jinsi alivyotendewa vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa kuteswa na kupigwa kikatili na pindi anapofika polisi hakuna hatua zozote zinazochukuliwa kwa mtuhumiwa huyo ambaye ni askari .
" Mimi niliolewa kwa ndoa na Stephen Kanyala ambae ni askari kitengo cha upelelezi ila baada ya kuolewa ukiwa umepita mwezi mmoja tuo nilianza kushuhudia mateso ya ndoa kutokana na kipigo na mateso makali niliyokuwa nikiyapata"
Anasema kuwa kila wakati pindi anapotaka kujua jambo kutokana kwa mume wake huyo hasa pale anapoona jumbe zenye utata katika simu yake ambazo zimetoka kwa wanawake anaiowatambua vizuri amekuwa akijibiwa kwa kipigo kikali. Rehema alisema kuwa ni rahisi kwake kuweza kuhesabia siku ambazo hajapigwa kuliko kuhesabi siku ambazo amepigwa ambazo ni nyigi zaidi .

" Kweli inasikitisha sana kusimulia kwani kabla ya kupigwa nimekuwa nikifungwa pingu mikono kama mharifu sugu na baada ya hapo kipigo kikali kimekuwa kikinikuta ....hadi sasa nimepigwa zaidi ya mara 20 na polisi nimekwenda kuripoti mara tatu na Hospital nimelazwa mara moja ila siku nyingine nimekuwa nikiugulia nyumbani ila nyumbani kwa wazazi nimerudi mara tatu sasa"
Alisema kuwa mbali ya kupigwa na kuumizwa ila kuna mateso mengine ambayo amekuwa akiyapata kutoka kwa mwanaume huyo ni siri yake na hayapaswi kuelezwa hapa kutokana na jinsi ambavyo askari huyo anavyomtenda ukatili wa kinyama. Hata hivyo alisema kuwa akiwa na mimba ya mwezi mmoja hali ya kipigo ilizidi zaidi na wakati mwingine alipata kumfunga shingo na kanga kwa kutaka kunyonga shingo huku akitishi kumuua,kinafafanua chanzo chetu cha habari hii.
Stephen Kanyala akiwa na mkewe wakati wa ndoa yao |
Hivyo alisema katika kunusuru uhai wake kwa sasa ameamua kurudi kwa wazazi wake na suala la ndoa hataki tena .
Kwa upande wake Mama mzazi wa Rehema akiwa Monica Shauri alisema kuwa amechoka kuuguza binti yake kwa kipigo na kuwa kuna wakati mwanaume huyo amekuwa akitishia kumpiga hata yeye.
Hivyo alisema kwa sasa mbali ya kumtoa binti yake Hospital ila wamekuwa wakiishi ndani wamejifungia milango kuogopa askari huyo kuja kuwafanyia ukatili ikiwa ni pamoja na kuwaua kwa risasi kama ambavyo amekuwa akiwatisha mara kwa mara kuwa dawa yao inachemka na ipo siku wataonja mauti.
Mama mzazi wa Rehema akiwa Monica Shauri
|
Bi Shauri alisema mbali ya kuwa yeye ni mmoja wa wacha Mungu kwa maana na Mlokole mzuri ambae kila wakati asubuhi lazima aende kusali ila kwa sasa anaogopa kutoka asubuhi kwa kuhofia kuvamiwa na askari huyo . Hivyo aliomba jeshi la polisi kuweza kumpa ulinzi yeye na familia yake ama kumkamata mtuhumiwa huyo ambae inadaiwa kwa sasa yupo katika mji wa Iringa ila askari wenzake wanamlinda.
Kuhusu uamuzi wa binti yake wa kuomba ndoa hiyo kuvunjwa alisema anaungana na binti yake kuikataa ndoa hiyo na kuwa kwa sasa wapo tayari kurudisha mahali yake ya Tsh 200,000 ambazo alizitoa kama mahali ili kunusuru uhai wao na uhai wa mtoto wake huyo.
0 your comments:
Post a Comment