![]() |
Striker James Chamanga wa Timu ya taifa ya Zambia akiangaliwa na Daktari wa Timu hiyo Kabungo baada ya kushambuliwa na mashabiki wa Ghana kwenye maegesho ya Magari |
Sep 6, 2013
Tagged under: Sport
Michezo| Mechi kati ya Ghana na Zambia Yaahirishwa baada ya Chipolopolo kufanyiwa fujo
Moja kati ya mechi kali za kufuzu kombe la Dunia mwakani nchini Brazil kwa bara la Afrika ambao ulitarajiwa kupigwa leo jioni kati ya Timu ya Taifa ya Zambia na wenyeji Ghana umeahirishwa baada ya wachezaji wa Timu ya Taifa ya Zambia kushambuliwa na kutokuhudumiwa ipasavyo na wenyeji wao,wakiwa katika mji wa Kumasi taarifa na Zibani Zambi
Mapema leo Timu ya Taifa ya Zambia ilishindwa kutembea Ghana huko katika mji wa Kumasi baada ya kukaidi mamlaka ya nchi hiyo kutokutua katika uwanja wa ndege wa Kumasi badala yake watue uwanja wa ndege wa kimataifa wa Accra,Serikali ya nchi hiyo imekilaumu chama cha soka cha Zambia(FAZ) na kusema kukaidi agizo ni ishara za kutoutendea haki mpira. Kwa mujibu wa chanzo cha habari hii unasema juhudi a kuutafuta uongozi wa shirikisho la kandanda la Zambia Football Association of Zambia (FAZ) ziligonga mwamba.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 your comments:
Post a Comment