300x250 AD TOP

Powered by Blogger.

Life & style

Popular Posts

Marafiki Waliotembelea Blog

Technology

NGOMA

Featured Video

UDAKU

Recent Posts

Popular Posts

Oct 8, 2013

Tagged under: , ,

Info| Psquare watajwa kuwa Wasanii wenye Utajiri zaidi Africa


Kupitia Post ya Mtandao wa Forbes iliyotumwa na Huffington imetaja List ya Wasanii 5 bora Tajiri Africa
Ifuatayo ndiyo List Kamili

1-Youssou N’dour
Msenegali  ambaye ndiye msanii Maarufu nchini Senegal na nje ya Mipaka ya nchi hiyo ndiye amepewa ukinara wa kuwa na Utajiri kuliko msanii yeyote,akitumia staili yake ya mbalax ambayo ni Mchanganyiko wa Nahadhi ya Kitamaduni tokea Senegal katika kabila la Serer,Cuban rumba, hip hop, jazz, nasoul,Youssou N’dour ametajwa kuwa Tajiri zaidi akiongoza kwa uwekezaji wa Pesa zake alizozipata kutokana na Mziki,Uwekezaji huo ni pamoja na kumiliki vyombo kamilifu vya Habari(Radio&TV) nchini Senegal.Kwa sasa Msanii huyo ni Waziri wa Utalii na utamaduni nchini humo alioupata mwaka 2012,kabla ya  K’naan kuipeperusha Bendera kwenye Kombe la Dunia 2010 na Wimbo wake maalum kwa Michuano hiyo Youssou alishawahi kufanya hivyo kwa kutunga wimbo maalum wa Kombe la Dunia mwaka1998 uliojulikana kwa jina la “La Cour des Grands,” akishirikiana na Axelle Red,Hata hivyo Chanzo cha Habari hii hakijaweka wazi N’dour anamiliki utajiri wa Kiasi gani


2-Psquare
Mapacha wa kufanana,Peter na Paul Okoye(P-Square) wametangazwa kushika nafasi ya Pili kwa utajiri,tokea wakiimba na kucheza utotoni mwao katika Kanisa moja la Kikatoliki huko Jos, Nigeria,baadae 2005 walipoamua kuunda kundi wakiwa Africa kusini wakafanya Vizuri Mara baada ya kupitia mikiki mikiki kadhaa na kufanikiwa kuuza kila Album waliyotoa kwa Mauzo ya Juu yakichagizwa na Maonyesho Mbali wanayofanya na kupelekea wakajitangaza zaidi Duniani ikiwemo kushirikiana na Wasanii wakubwa kama vile Akon ikapelekea wasanii hawa kutangazwa wasanii Bora wa Mwaka 2010 kupitia Tuzo za Kora tendo lililowafanya waanze kulipwa $150,000 kwa show,Zaidi ya yote wanautajiri unaosemekana ni zaidi ya $3 million huku wakimili eneo lenye thamani kubwa nchini Nigeria la “Squareville.” na Baadhi ya Thamani kama Magari,ndege,Boats ya Gharama.

3-DBANJ
Akianza Mwaka 2007 kuitikisa Nigeria na Dunia kwa Ujumla D’banj, aka the Koko Master, aka Dapo Daniel Oyebanjo,ambaye kwa sasa akiwa ni msanii pekee toka Africa kusaini lebel ya GOOD MUSIC ya Marekani iliyo chini ya Kanye West,Mwenye mafanikio ya kubeba Tuzo zisizohesabika  kwa Mujibu wa Chanzo cha Habari hizi ametangazwa kuwa msanii namba 3  kwa Utajiri Africa kutokana na Mafanikio yake ya Mziki akimiliki Club moja kubwa nchini Nigeria,Kampuni ya Maji ya kunywa(Koko water),pamoja na na kipindi kimoja cha Television  “Koko Mansion.”







4. Koffi Olomidé
Akiwaibua Mastaa kadhaa wa Kikongo akiwemo  Fally Ipupa, Koffi Olomidé formed Quartier Latin mwenye sauti ya Kipekee ikichagizwa na staili ya uimbaji na uchezaji ifahamikiayo kama Vas tcha tcho ambayo imefanya akajulikana ulimwenguni na kupelekea msanii huyu kufanya kila show kwa gharama ya 100,000 euros,Koffi ametajwa kushika namba 4 kuwa Msani mwenye utajiri zaidi Africa,,Historia anayojivunia ni kuandikwa kwenye  Robert Dimery chenye maelezo yakielezea jinsi Album 1001 za Koffi ambazo si zakukosa kuzisikiliza “1001 Albums You Must Hear Before You Die.”

5. Salif Keita
Alizaliwa na kukulia nchini Mali,ni mwimbaji na mwandishi wa nyimbo pia,Salif Keita cha kujivunia toka kwake ni jinsi anavyoitumia vizuri auti yake iliyosababishwa akapewa hadhi ya mmiliki wa sauti halisi toka Afrika(Golden Voice of Africa),anaimba mziki wa Afro-pop,anatoka katika koo ya Kifalme ya Sundiata Keita,koo ambazo ndiyo waanzilishi wa Falme ya Mali( Mali Empire),alijiingiza katika mambo ya Mziki,Kabla hajaacha kazi ya Mziki msanii huyo alikuwa tayari Mziki umemwingizia kipato cha kutosha kilichomfanya akamiliki kisiwa kimoja huko Ulaya,Salif Keita ametangazwa kushika nafasi ya 4 kwa Utajiri barani Africa.

Habari njema kwa Afrika Mashariki msanii Jose Chameleone toka Uganda anapigiwa Kura ya kuwepo kwenye 10 bora,swali ni jee Tanzania utajiri wa wasanii wetu hauwezi kufanya wasanii wetu kuwepo kwenye 10 Bora??? .

0 your comments:

Post a Comment