
Ukifungua simu ya Mesut Ozil utakutana na meseji za Jose Mourinho. Zipo nyingi, japo Ozil ameamua kuiweka hadharani meseji moja, inayosomeka kwa kimombo ‘Welcome to London’ kwa maana ya ‘karibu London’.
Meseji nyingine walizotumiana wawili hao ni siri
yao. Ozil amesema hivyo. Haijulikani kama Mourinho anatuma meseji za
aina gani kwa Ozil hasa kwa kipindi hiki anachoonyesha uwezo mkubwa wa
soka katika klabu yake mpya ya Arsenal.
Kiungo huyo Mjerumani, Ozil msimu huu ameuanza kwa
kasi kubwa akiwa ndani ya jezi za Arsenal baada ya kujiunga katika
dakika za mwisho za siku ya kufunga usajili akitokea Real Madrid, mahali
ambako alikuwa pamoja na kocha Mreno, Mourinho.
Mourinho mambo yake hayapo vizuri sana katika
klabu yake ya Chelsea kwenye Ligi Kuu England na huwezi kujua nini
mpango wake wa Januari mwakani baada ya mwaka huu kumkosa straika
aliyekuwa akimwinda kwa nguvu zote, Wayne Rooney.
Ozil amesaini mkataba mrefu ndani ya Arsenal,
lakini kwa mchezaji wa kariba yake ni lazima kikosi hicho cha Arsene
Wenger kihakikishe kwamba hakitoki kapa kwenye kutwaa mataji kwa misimu
isiyozidi miwili, vinginevyo kila kitu kitakuwa tofauti.
Mourinho ni kocha mwenye nguvu sana na si mtu
anayemtakia mema Wenger baada ya kuzuia uhamisho wa straika Demba Ba
katika dakika za mwisho, alipogundua Mfaransa huyo amemnasa kiungo mkali
wa pasi fupi za mwisho, Ozil.
Jose amtumia meseji, Ozil afanya siri
Kuna kitu kinatia wasiwasi juu ya meseji
wanazotumiana Mourinho na Ozil kwa sababu staa huyo wa Ujerumani
anafanya siri licha ya kwamba si jambo zuri kutaka kufahamu ni kitu gani
wanachozungumza wawili kwa sababu ni mambo binafsi.
Mourinho kiukweli ana wivu kwa kumwona Ozil
akifanya mambo kwenye kikosi cha Arsenal, inayonolewa na kocha ambaye
daima hawakuwa na uhusiano mzuri tangu awamu ile ya kwanza aliyokuwa
Chelsea hadi sasa aliporejea tena kwenye klabu hiyo ya Stamford Bridge.
“Ndiyo, kuna mambo tunawasiliana. Alinitumia SMS
akisema ‘karibu London’,” alisema Ozil alipozungumza na gazeti la Bild
la Ujerumani.
Hata hivyo, baadaye akasema “mengine yanatuhusu
wenyewe,” wakati alipoulizwa swali ni meseji za aina gani anazotumiwa na
kocha wake huyo wa zamani katika Uwanja wa Santiago Bernabeu.
Imebainika kwamba hadi dakika za mwisho kwenye siku ya mwisho ya kufungwa kwa dirisha la usajili Ulaya, kiungo huyo alikuwa akifanya mazungumzo na klabu ya Manchester United.
Ozil amezipokea kauli za Rais wa Real Madrid, Florentino Perez
kwamba asingeweza kumudu presha ya kushindania namba kwenye kikosi hicho
kinachonolewa na Carlo Ancelotti kwa sasa.
Wakati mashabiki na wachezaji wenzake wa zamani
katika kikosi hicho wakiwa na mapenzi makubwa na staa huyo, Ozil amekiri
kuwa na bifu na klabu hiyo hasa viongozi wake.
Kuthibitisha hilo, staa huyo wa Ujerumani alisema
kwa sasa amekata kabisa mawasiliano na timu hiyo na kwamba kwenye maisha
yake ya soka kwa sasa Real Madrid ataishukuru kwa kumtengenezea
historia na kumwezesha kucheza Ligi Kuu kubwa tatu Ulaya, baada ya
kung’ara Bundesliga, La Liga na sasa Ligi Kuu England.
Mwenyewe aichagua Arsenal
Mwenyewe aichagua Arsenal
![]() |
Per Mertersacker kushoto akiwa na Ozil Mazoezini |
Imebainika kwamba hadi dakika za mwisho kwenye siku ya mwisho ya kufungwa kwa dirisha la usajili Ulaya, kiungo huyo alikuwa akifanya mazungumzo na klabu ya Manchester United.
Klabu hiyo inayonolewa na David Moyes ilikuwa
kwenye kampeni za kumhitaji staa huyo, kabla Wenger hajatumia uzoefu
wake kwa kumpigia simu Ozil na hatimaye kufanikiwa kuipata saini yake.
Baada ya kuonja benchi Real Madrid, Ozil aliamua
kuchagua kwenda Arsenal iliyochini ya Wenger mahali ambapo kuna
Wajerumani wengine, Per Mertersacker na Lukas Podolski ambao inadaiwa
walichangia kwa namna fulani kumshawishi kiungo huyo kutua Emirates.
Hata hivyo, kitendo cha kufuatwa na Manchester
United na kufanya nao mazungumzo hadi dakika za mwisho, kisha akaichagua
Arsenal ni ishara kwamba mchezaji huyo amefanya uamuzi ambao
haukushawishiwa na pesa licha ya kwamba Arsenal ililipa Pauni 42.5
milioni kumnasa, huku ikimhakikishia mshahara wa nguvu.
Hadi sasa zikiwa zimechezwa mechi saba tu kwenye Ligi Kuu, Ozil ameonyesha cheche za nguvu na kuifanya Arsenal kuongoza ligi.
Kwa namna ilivyo, usajili wa Ozil utakuwa na faida
kubwa muhimu kwa Arsenal kwa sababu moja, staa huyo atataka kuwaonyesha
waajiri wake wa zamani, Real Madrid wanaodai kwamba mchezaji huyo hana
jipya na wala hawajutii kumpoteza yeye ni mtu muhimu na kiwango chake
kipo juu.
Ugomvi huo na mabosi wake wa zamani utakuwa na faida kubwa kwa
Arsenal kwa kuwa wataendelea kuvuna mambo ya maana kutoka kwake
anapokuwa uwanjani.
Hadi sasa Mjerumani huyo amepika mabao matano
katika mechi sita za Arsenal na kuwasaidia kutamba Ligi Kuu na kuongoza
pia Kundi F kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.
SOURCE:
Mwanaspot
0 your comments:
Post a Comment