Katibu
Mtendaji wa Mpango wa Afrika Kujitathmini Kiutawala Bora (APRM) Tanzania Rehema
Twalib (wa kwanza kushoto) akiongea na waandishi wa habari leo jijijni Dar es
salaam ambapo Tanzania inaungana na nchi nyingine za Afrika wanachama wa mpango
huo kuadhimisha siku APRM na kutoa taarifa ya tathmini ya utawala bora nchini.
Katikati ni Afisa Habari Idara ya Habari MAELEZO Frank Mvungi na wa kwanza
kulia ni Mratibu wa APRM Tanzania Dkt. Cuthbert Ngalepeka.
Katibu
Mtendaji wa Mpango wa Afrika Kujitathmini Kiutawala Bora (APRM) Tanzania Rehema
Twalib (wa kwanza kushoto) akiongea na waandishi wa habari leo jijijni Dar es
salaam kuhusu hatua zilizofikiwa na Serikali ya Tanzania kutekeleza majukumu
yake kwa mujibu wa mkataba wa Afrika wa tathmini ya APRM. Pamoja kuzungumzia
masuala ya kitaifa hususani mchakato wa katiba unaoendelea. Wa kwanza kulia ni Afisa
Habari Idara ya Habari MAELEZO Frank Mvungi.
KatibuMtendaji wa Mpango wa Afrika Kujitathmini Kiutawala Bora (APRM) Tanzania Rehema
Twalib (wa pili kushoto) akiongea na waandishi wa habari leo jijijni Dar es
salaam ambapo alisema kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi 34 kati ya 54
zilizojiunga na mpango wa APRM na kuwashirikisha wananchi kutoa maoni yaokuhusu
hali ya utawala bora nchini. Wa kwanza kushoto ni Afisa Mawasiliano wa APRM
Hassan Abbasi.
Baadhi
ya waandishi wa habari wakitekeleza majukumu yao leo jijini Dar es salaam ambapo
Tanzania inaungana na nchi nyingine za Afrika wanachama wa Mpango wa Afrika
Kujitathmini Kiutawala Bora (APRM) katika kuadhimisha siku ya APRM na
kutoa taarifa ya tathmini ya utawala
bora nchini. (Picha zote na Eleuteri Mangi -MAELEZO)
Tanzania
yaendelea kuwa kinara wa Utawala bora
Na
Frank Mvungi-MAELEZO.
MPANGO
wa Afrika wa kujitathmini kiutawala bora (APRM) umebainisha kuwa Tanzania ni
moja ya Nchi zinazofanya vizuri katika utawala
bora.
Hayo
yamesemwa na Katibu Mtendaji wa APRM Tanzania Rehema Twalib wakati wa mkutano
na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam alipokuwa akieleza mafanikio
yaliyofikiwa hadi sasa ikiwa ni sehehmu ya maadhimisho ya siku mchako huo ambayo
huadhimishwa Machi 9 kila mwaka.
Bi
Rehema alibainisha kuwa Tanzania imepata mafanikio katika Nyanja za Demokrasia
na Utawala Bora, Siasa, Usimamizi wa uchumi, uendeshaji wa makampuni,Maendeleo
ya uchumi-Jamii na Masuala mtambuka kama afya.
Akifafanua
zaidi Bi. Rehema alisema Tanzania kupitia APRM imefanya tathmini yake katika
maeneo hayo na kuwasilisha ripoti yake mbele ya wakuu wa nchi wanachama na
kujadiliwa.
Wakati
huo huo alizitaja hatua zinazochukuliwa na Serikali kuwa ni kuanza kufanyia
kazi mpango kazi wa kitaifa (NPoA) wa kuondoa changamoto zilizobainishwa katika
ripoti ya APRM kuhusu hali ya utawala bora nchini.
Pia
Bi Rehema alizitaja hatua nyingine ambazo Tanzania imefikia katikakutekeleza mchakato wa APRM kuwa ni kuwashirikisha
wananchi kutoa maoni yao kuhusu hali ya utawala bora nchini na Serikali
kuruhusu wataalamu wa utawala bora kutoka nchi wanachama kuja nchini kuhakiki
mchakato huo.
Aidha,
Bi Rehema alibainisha kuwa lengo kuu la mpango huu ni kuwashirikisha wananchi
ili kushirikiana na Serikali zao kubaini changamoto za utawala bora ili
zifanyiwe kazi na kuhimiza nchi kutekeleza viwango vinavyokubalika kimataifa na
kikanda.
APRM
ni mpango ulioasisiwa machi 9, 2013 na wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika (AU)
ambapo Tanzania kwa sasa ni miongoni mwa nchi 34 kati ya 54 za AU zilizokwisha
jiunga na mpango huu ambapo ilijiunga mwaka 2004.
Source:Jiachie Blog
0 your comments:
Post a Comment