Misaada iliyotolewa na Access kwa wateja wao |
Benki ya Access tawi
la Kahama imeamua kusherehekea sikukuu
ya Pasaka kwa kutoa msaada kwa wajasiriamali 11 toka kijiji cha Mwakata ambao
pia ni wateja wao, waliokumbwa na janga la mvua ya mawe iliyouwa watu 47 na
kujeruhi wengine 112.
Meneja wa Access Bank tawi la Kahama Hussein Kapilima aliyevaa tshirt nyeupe kulia kwake ni Meneja wa benki hiyo kanda ya Magharibi Prosper William katika picha ya pamoja na wateja wao |
Akikabidhi msaada huo
Meneja wa benki hiyo kanda ya Magharibi Prosper William amesema benki ya Access
imeguswa na kilichotokea mwakata hivyo kwa kutambua umuhimu wa wateja wao
wameamua kuungana kusherehekea Pasaka na wahanga hao.
Prosper amesema
kushirikiana na jamii ni moja ya wajibu
wa Benki hivyo kilichowakumba watu wa Mwakata wakiwemo wateja wao kimewagusa
pia na ndiyo maana wameamua kusherehekea nao Pasaka na kuahidi kuwa benki
itaendelea kushiriki kwenye masuala jamii.
Jengo la Ofisi ya Access Bank tawimla Kahama |
Naye Meneja wa benki
hiyo tawi la Kahama Hussein Kapilima amesema benki inabidi kubadilisha
mashariti ya huduma kwa wateja hao kwani hali iliyopo kwa sasa eneo la Mwakata
inawawia vigumu hata wateja wao kuyamudu masharti hayo.
Kwa upande wake
diwani wa kata ya Mwakata Ibrahim Masanja kwa niaba ya wajsiriamali hao
ameishukuru benki hiyo kwa kushiriki nao katika Pasaka na kuiomba iendelee kuwakumbuka katika masuala mengine
ikiwemo kuwapunguzia masharti katika huduma wanazozitoa.
Msaada uliotolewa na
benki ya Access kwa wajasiriamali hao ambao ni wateja wa benki hiyo ni kilo 110
za Maharage,kilo 110 za Mchele,Boksi 42 za Sabuni,na Dagaa debe 22, msaada
wenye thamani ya shilingi milioni 1.
Wateja wa benki ya Access toka kijiji cha Mwakata kilichokumbwa na janga la mvua iliyoambatana na upepo mkali,wakiwa katika ofisi za benki hiyo kupokea msaada |
0 your comments:
Post a Comment