|
Afisa
mtendaji mkuu wa Diamond
Trust Bank Tanzania Limited(DTB) bi Nasim Devji akizungumza wakati wa
uzinduzi wa tawi la DTB Kahama ambapo alisema hivi sasa DTB hivi sasa
ina matawi 23 nchi nzima,matawi 10 yapo jijini Dar es salaam,mawili yapo
jijini Arusha |
Leo Alhamis,April 2,2015 afisa mtendaji mkuu wa Diamond
Trust Bank Tanzania Limited(DTB) bi Nasim Devj amezindua tawi jipya la benki
hiyo lililopo katika barabara ya Ngaya/Isaka mjini Kahama mkoani
Shinyanga,ambapo watu mbalimbali kutoka ndani na nje ya Tanzania wamehudhuria
uzinduzi huo.Tawi la Kahama ni la tatu katika kanda ya Ziwa(mengine yapo Mwanza
na Tabora) lengo likiwa ni kuhudumia jamii ya wafanyabiashara nchini Tanzania.
Mkurugenzi
wa DTB Tanzania bwana Mehboob Champsi alisema akiba za wateja zimekua
kwa asilimia 44.5 kutoka Tzs 399.7 bilioni mwaka 2013 hadi Tzs 577.5
bilioni,wakati mali za benki zimefikia Tzs 690.0 bilioni ikionesha
ukuaji wa asilimia 36.4 kwa mwaka 2014 kutoka Tzs 505.7 bilioni kwa
mwaka 2013
DTB
inakuwa benki ya 10 ya kibiashara kufungua milango yake katika wilaya
ya Kahama huki ikitoa huduma kamili za kibenki kwa watu wa Kahama
PICHA KATIKA MATUKIO KWENYE HAFLA HIYO.
|
Afisa
mtendaji mkuu wa Diamond
Trust Bank Tanzania Limited(DTB) bi Nasim Devji akimkabidhi zawadi meneja wa DTB tawi la Kahama Mercy Stephen |
|
Afisa
mtendaji mkuu wa Diamond
Trust Bank Tanzania Limited(DTB) bi Nasim Devji akisaini kitabu cha wageni |
|
Bi Sheribanu Kurji ambaye ni mama mzazi wa
afisa
mtendaji
mkuu wa Diamond Trust Bank Tanzania Limited(DTB) bi Nasim Devji akikata utepe kufungua tawi la beki hiyo wilayani Kahama.
|
|
Afisa
mtendaji mkuu wa Diamond
Trust Bank Tanzania Limited(DTB) bi Nasim Devji akimlisha Cake meneja wa benki hiyo tawi Kahama. |
|
Wakati wa maakuli hapa waandishi wa habari nao wakijumuika katika chakula katika hafla hiyo. |
|
Kadama Malunde wa Malunde1 Blog naye alikuwepo akifanya yake pembeni ni Paul Kayanda wa gazeti la Mtanzania |
0 your comments:
Post a Comment