300x250 AD TOP

Powered by Blogger.

Life & style

Popular Posts

Marafiki Waliotembelea Blog

Technology

NGOMA

Featured Video

UDAKU

Recent Posts

Popular Posts

Nov 6, 2015

Tagged under: , , , ,

Infor| ITV Tanzania kutambulisha kipindi Kipya jumatatu ya Novemba 9 mwaka huu

LOGO ya Kipindi hicho
Kituo cha Runinga hapa nchini chenye hadhi ya Runinga bora zaidi Afrika Mashariki(Super Brands')ITV kimeboresha uwasilishaji wa Matangazo yake kwa kuongeza kipindi kipya ambacho kinataraji kuanza kuruka Jumatatu ya tarehe 9 Novemba 2015.
Kipindi hicho kilichoongezwa kinakwenda kwa jina la THE BASE ambacho kitakuwa kikiongozwa na Aloy Sazia(Mapembe) na jopo la wasaidizi katika kipindi hicho.
Aloy Sazia a.k.a Mapembe aliyeshika MIC
Mwendesha kipindi THE BASE SHOW Aloy Sazia Mapembe
Kwa mujibu wa mwendesha kipindi hicho Mapembe amesema Kipindi hicho ni cha burudani kikihusisha mziki,harakati  mtaani za maisha ya wasanii na akaongeza kuwa huu ni ujio mpya wa burudani ambao vijana wengi wataguswa kwa kupata elimu juu ya maisha ya watu wanaowakubali.
Moja ya picha za uaandaaji wa kipindi hicho
Hatua za mwisho za uaandaaji wa kipindi hicho zimekamilika hivyo kinachosubiriwa ni  kuanza kwenda hewani siku ya jumatatu wiki ijayo saa 11 jioni.
Aloy Sazia Mapembe wa mwanzo kulia kwako,akiwa na jopo la THE BASE SHOW
Kwa muda sasa mwendesha kipindi hicho Aloy Sazia Mapembe kupitia ukurasa wake wa Facebook amekuwa akiweka picha tofautitofauti zikiwa na maelezo ya mwendelezo wa uaandaaji wake.
Aloy Sazia a.k.a Mapembe aliyeshika MIC
Kila la kheri ITV kwa kutambua haja za watazamaji wenu mkaamua kupanua wigo wa Matangazo kwa kuongeza kipindi ambacho hakika mtaongeza watazamaji wengi.

0 your comments:

Post a Comment