
Hatimae wekundu wa msimbazi wamefanikiwa kuinasa saini ya aliekuwa mshambuliaji nguli wa klabu ya Azam FC baada ya kufikia makubaliano na uongozi klabu hiyo.Ngassa aliekuwa mchezaji wa klabu ya
Azam takribani misimu miwili,alipojiunga nayo akitokea klabu ya Yanga.
Mbali na saini hiyo pia uongozi wa Simba umempatia mshambuliaji huyo mpya kunako kikosi kinachojiandaa na mikikimikiki ya ligi kuu ya vodacom tanzania bara inayotarajia kuanza mapema mwezi wa nane gari ambalo litamsaidia mshambuliaji huyo katika shughuli zake mbali mbali ikiwemo za michezo.
Mshambuliaji huyo ameinufaisha klabu ya Azam kitita cha mililion 25 za kitanzania kama ada ya uhamisho wa mchezaji huyo tokea klabu yake aliyokuwa akiichezea kwenda simba
0 your comments:
Post a Comment