![]() |
Victor Wanyama |
Kiungo wa timu ya taifa ya Kenya Harambee Stars anayekipiga katika klabu ya Celtic ya Scotland Victor Wanyama amesita kutoa mustakabali wake kuhusiana na kuongeza mkataba mpya ama laa.Mkataba wake unatarajia kuisha mwaka 2015 jambo ambalo linaikosesha usingizi management ya Celtic jinsi ya kumbakisha kundini kinda huyo wa taifa la Kenya mwenye umri wa miaka 21 tuu.
Victor hivi majuzi amehusishwa na tetesi za kutimkia Oldtrafford-Manchester United ya Uingereza ambayo imeonesha nia ya kumchukia kiungo huyo.Wanyama alijiunga na Celtic mwaka 2011 akitokea klabu ya Beerschot ya Ubelgiji na kusema kuwa hadhani kama mkataba mpya unaweza kumlipa kutokana na kazi anayoifanya klabuni hapo ni bora akatimkia kwingine kimaslahi zaidi.
Naye wakala Rob Moore amezungumzia mipango ya mchezaji wake na kusema ujira anaolipwa Wanyama hauendani na kazi anayoifanya klabuni hapo
0 your comments:
Post a Comment