Moja ya wanajeshi wa Congo akiwa kazini kuwadhibiti Waasi katika eneo la Goma-kaskazini mwa Congo |
Taarifa za awali zilizothibitishwa na msemaji mkuu wa Nchi hiyo bw.Lambert Mende zinasema wapiganaji wapatao 51 waliuawa huku wakiwa wamevalia sare za jeshi la Rwanda jambo ambalo serikali ya Rwanda wamekanusha kuhusiana na tuhuma za awali zinazodai kuwa Taifa hilo linawaunga mkono waasi hao kutokuhama katika eneo hilo lenye utajiri mkubwa wa Madini.
Umoja wa matifa unazishutuma nchi za Rwanda na Uganda kuhusika na mapigano ya mara kwa mara ambayo mpaka leo ijumaa yanaendelea kaskazini mwa mji wa Goma katika eneo la Kibumba.Hali si shwari katika eneo hilo huku wakazi wakilazimika kuyahama makazi yao kuelekea katika vitongoji vilivyoko kaskazini magharibi mwa Goma ambako ndiko kuna kambi kubwa ya wakimbizi ya Kibai.
Baadhi ya matukio ya mapigano kati ya Waasi na Majeshi ya Umoja wa Mataifa yanayoisaidia Congo kukabiliana na Waasi. |
0 your comments:
Post a Comment