vijana wa Serengeti Boys wakiomba kwanza kabla ya mazoezi |
Kocha wa makipa wa Serengeti Boys Peter Manyika akitoa maelekezo kwa wachezaji wake katika mazoezi yaliyofanyika hii leo jioni uwanja wa Taifa |
kocha mkuu wa Serengeti Boys Jacob Michelsen akitoa maelekezo ya vitendokwa vijana wake |
Serengeti Boys wamefanikiwa kufuzu raundi ya tatu kufuatia ya hasimu wake katika raundi ya kwanza na ya pili timu za Kenya na Misri ambazo zingecheza na vijana hao wa Michelsen kujitoa katika kuwania kufuzu kwa michuano hiyo.Mwaka 2005 Serengeti Boys walifanikiwa kufuzu katika michuano hiyo iliyofanyika nchini Gambia lakini hawakuweza kushiriki kufuatia shirikisho la mpira wa miguu afrika(CAF) kufungia timu hiyo kwa udanganyifu wa umri kwa mchezaji Nurdin Bakari.
Peter Manyika Peter mlinda mlango namba 1 wa Serengeti Boy |
Kocha Michelsen ameongeza kuwa licha ya kuwa nyumbani mchezo huo utaenda kuwa mkali huku akiweka wazi wapinzani wake wanawachezaji waliozidi umri(vijeba) kwani katika timu hiyo ya Congo kuna baadhi ya wachezaji waliokwenda nchini Mexco kushiriki michuano ya kombe la dunia U-17 ambapo timu hiyo ilweza kutolewa kunako raundi ya pili huku akiwataja baadhi ya wachezaji ambao anawatilia shaka kuwa ni pamoja na Chaverly Mabiat na Hady Binguila.
magolikipa-Serengeti Boys wakiwajibika mazoezini |
Manyika Peter baba wa Peter Manyika |
0 your comments:
Post a Comment