300x250 AD TOP

Powered by Blogger.

Life & style

Popular Posts

Marafiki Waliotembelea Blog

Technology

NGOMA

Featured Video

UDAKU

Recent Posts

Popular Posts

Nov 20, 2012

Tagged under:

MATUKIO:WAASI WA M23 WAUTEKA MJI WA GOMA KASKAZINI MASHARIKI MWA CONGO.

Waasi wa M23
Wafuasi wa wapiganaji wa M23 wamefanikiwa kuingia katika mji mkuu wa mashariki mwa Congo(Goma),mji wenye utajiri mkubwa wa madini.Duru za habari duniani zinasema kuwa wafuasi hao toka M23 wamefanikiwa kuingia eneo hilo baada ya kuwazidi nguvu wanajeshi wa serikali walipokuwa katika majibizano ya risasi.Kufuatia mapigano hayo maelfu ya raia wa Congo wameyakimbia makazi yao mapigano ambayo yamezua taarifa kwamba huenda mapigano yakazuka tena upya katika nchi ya Kidemokrasia ya watu Congo huku taarifa zikiweka wazi kwamba tangia mapigano hayo yaanze takribani watu million tano wamepoteza maisha.
Wafuasi wa M23 wamefanikiwa kuingia katika eneo la Goma kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2003 ambapo mapigano hayo yaliripotiwa kumalizika.Huku jeshi la umoja wa mataifa la kutunza amani likikanusha kuwepo taarifa za wafuasi wa M23 kumiliki uwanja wa ndege.
Baadhi ya raia wa  DRC-Congo wakikimbia mapigano kati ya majeshi ya serikali na waasi wa M23
Awali Serikali ya Kidemokrasia ya Congo ilipuuza taarifa za waasi wa M23 kudai kuanzisha mazungumzo ya amani na kusema yenyewe itaendelea kulilinda eneo hilo la mashariki mwa nchi hiyo la Goma.Nayo serikali ya Rwanda imekanusha kuhusika kuwaunga mkono wapiganaji wa M23 katika mapigano hayo.
Haya ni mapigano mabaya zaidi kuripotiwa kutokea tangu Julai mwaka huu mashariki mwa Kidemokrasia ya Congo huku baraza la usalama wa Mataifa likilaani hatua hiyo ya waasi wa M23 kufika katika eneo la Goma eneo lenye utajiri mkubwa wa madini.

0 your comments:

Post a Comment