Hapa Snoop Lion zamani Doggy akiwa na marafiki zake kwenye uzinduzi wa FIFA13. |
''Nina mapenzi makubwa na soka,hii si mara ya kwanza kwa nyota kuwekeza katika timu mbalimbali za michezo lakini hii ni mara ya kwanza kwa nyota kama mimi kuwekeza katika mpira wa miguu'' alisema Snoop na kuongeza kuwa 'sikuiangalia mechi ya Celtic na Barcelona lakini nilipata nafasi ya kuona marejeo ya mchezo huo,Barcelona ni timu kubwa lakini kwa sasa Celtic ni timu nzuri pia kwangu.Nilona jinsi mashabiki walivyokuwa na mapenzi na timu yao na mimi nimeona niwekeze katika moja ya bodi kwenye klabu hiyo.
Sitaki kuelezea ni kiasi gani nitawekeza na sihitaji kuimiliki klabu yoyote ya mpira ila kwa asilimia chache ambayo bodi ya timu wakiihitaji ntawasikiliza,nahitaji kuweka chochote katika klabu hiyo japo kwa uchache',alitanabaisha hayo pindi alipokuwa akifanya mahojiano na mtandao wa the Daily Record.
Kabla haujafikiria zaidi juu ya uamuzi wa Snoop Lion zamani Snoop Doggy fahamu kwamba mwaka 2005 aliweza kuonekana katika moja ya picha zikimwonesha amevalia jezi ya klabu ya Celtic na hapo tayari alikuwa amemwulizia swahiba wake msukuma gozi raia wa Uingereza David Beckham kuhusiana na Celtic ambapo alijibiwa na Beckham kuwa 'hii timu haitakuwa klabu kubwa',
Snoop akiwa katika vazi ambalo kwa ndani kaweka t-shirt ya klabu ya Celtic |
Snoop Lion hakusita kumzungumzia mchezaji Giorgos Samaras kuwa ni mchezaji mwenye kipaji 'nampenda Samaras ni mcheza mpira mzuri na hatari na kama tunahitaji kufika mbali basi yampasa acheze vizuri',maelezo ambayo yameweza kumweka katika hali nzuri(morali)Samaras.
Giorgos Samaras akiwa mazoezini. |
0 your comments:
Post a Comment