Ndani ya kanisa hilo |
Akizungumza na vyanzo vya habari hii,Afisa mmoja wa baraza la mji huo amesema kuwa kumetokea milipuko ndani ya jengo la kanisa hilo wakati watu wanne wanaosadikika kuwa ni waumini walipokuwa wakipata chakula,ambapo pia ameongeza kuwa shambulio hilo lilikuwa la kujitengenezea,kwani baruti zilizohusika ni zile ambazo hutumiwa na wavuvi.
Naye waziri wa mambo ya nje wa Misri bw.Mohammed Kamel Amr amesema kuwa Serikali ya nchi hiyo imeagiza uchunguzi wa kina ufanyike na wataokamatwa kuhusika na shambulio hilo watachukuliwa hatua.Kanisa hilo lililoko eneo la Dafiniyah mjini Misrata hutumiwa na raia wengi wa Misri kufuatia na kuwepo na idadi ndogo ya wakristu nchini Libya wengi wao wakiwa ni wa kigeni hususani toka nchini Misri ambao hufanya ibada katika dhehebu hilo ambalo ndilo dhehebu pekee kubwa nchini Libya.
Viongozi wa kanisa la Coptic wakiwa katika sala. |
Moja ya jengo yaliyobomolewa na shambulio hilo mjini Misrata |
0 your comments:
Post a Comment