Moja ya vikao vya mahakama ya ICTR |
Mahakama ya Kiamataifa inayoshughulikia kesi ya mauaji ya Kimbari ya Rwanda leo imetoa hukumu kifungo cha kwenda Gerezani miaka ipatayo 35 kwa mmoja kati ya wale washukiwa kuhusika kwa mauaji hayo anayekwenda kwa jina la Augustin Ngirabatware ambaye aliwahi kuwa waziri wa Mipango wa Serikali ya Kihutuiliyokuwa madarakani wakati mauaji hayo yakitokea.
Idadi ya Raia wa Rwanda makabila ya Watusi na Wahutu wapatao laki nane walipoteza maisha kufuatia mapigano hayo ya wenyewe kwa wenyewe yakichukua takribani siku miamoja nchini Rwanda mnamo mwaka 1994.
Bwana Augustin Ngirabatware amekuwa mtu wa mwisho kufunguliwa mashtaka katika mahakama ya Kimataifa yanayoshughulikia mauji ya Kimbari ya Rwanda maarufu kama ICTR yenye makao makuu yake jijini Arusha nchini Tanzania ambayo kwa leo ndiyo itaanza kusikiliza kesi za rufaa.
Kupitia kwa jaji wa Mahakama hiyo William Hussein alisema''Mahakama hii imekuhukumu kifungo cha miaka 35 Gerezani kwa uhalifu ulioutenda'',Ngirabatware alikutwa na hatia ya kuhusika na mauaji,kuchochea wapiganaji wake kuhusika na mauaji ya halaiki,ubakaji na ukatili tofautitofauti dhidi ya Binadamu.
moja ya mabaki ya miili ya watu waliokufa katika mapigano ya wenyewe kwa wenyewe kati ya Watusi na Wahutu nchini Rwanda mwaka 1994 |
Inatazamiwa hadi kufika mwaka 2014 mahakama hiyo itasitisha shughuli zake baada ya kusikiliza kesi za rufaa zipatazo 16 zilizo wasilishwa mbele yake.
Mmoj Y waathiriwa wa mapiganohayo akionesha baadhi ya alama za makovu aliyoyapata wakati wa mapigano |
BAADHI YA PICHA ZA MABAKI YA WALIOATHIRIKA NA MAUAJI YA KIMBARI YA RWANDA YA MWAKA 1994
0 your comments:
Post a Comment