300x250 AD TOP

Powered by Blogger.

Life & style

Popular Posts

Marafiki Waliotembelea Blog

Technology

NGOMA

Featured Video

UDAKU

Recent Posts

Popular Posts

Dec 31, 2012

Tagged under: , , , , , ,

MSANII BRITNEY SPEARS AJIKITA ZAIDI KWENYE MZIKI

                Akijibu maswali ya mashabiki wake kupitia mtandao wa Twitter hapo jana Msanii Britney Spears alisema kuwa anafanya kazi kwa kujituma kuhakikisha anakamilisha Album yake ya 8 huku akiongeza kuwa kwa sasa analenga zaidi katika masuala ya mziki na awamu hii anataka kufanya kazi na waandaaji wa mziki(producers) wapya ambao kwa wanamvutia kiutendaji.
                   Katika swali lilioelekezwa kwake kupitia mtandao huo wa kijamii likisomeka hivi
''@britneyspears,can we expect it to be out in 2013?Excited for next album for Britney!'',
''@BritneyUKSpears,,Really focused on my music right now'',aliweza kutweet kama hivyoakijibu baadhi ya maswali yaliyokuwa yakielekezwa kwake na mashabiki wake toka UK.
Britney Spears katika moja ya pozi
             Mwezi uliopita mwanadada huyu aliweza kufanya collabo na mmoja kati ya members wa kundi la Black Eyed Peas mwite will.i.am katika ngoma inayokwenda kwa jina la Scream & shout na katika harakati hizo msanii huyo ameliorodhesha kwenye list jina la mwandishi wa nyimbo Elijah Blake ambaye ndiye aliyeandika ngoma ya Usher Raymond inayofahamika kwa jina la ''Climax''

                Album ya mwisho ya Spears inayokwenda kwa jina la Femme Fatale iliyobeba nyimbo zilizofanya vizuri kama vile Hold It Against Me iliyoshika namba 1 katika chat za BillboardTop100,Till The World Ends iliyowahi kushika namba 3 katika chat za billboardTop100,I Wanna Go iliyokaa katika namba 7 kwenye chat hizo za Billboard.
        Kwa mujibu wa mtandao wa kiburudani unaoshughulika na masuala ya wasanii nchini Marekani(NielsenSoundScan) iliweza kuuza nakala(copies) 276,000 ndani ya wiki yake ya kwanza ya mauzo na ikiwa Album iliyoshika namba 1 kwenye chat za BillboardTop200 mwaka jana.Matazamio yake anategemea Album yake hiyo ijayo itakuja kufanya vizuri zaidi kwani anatarajia kuifanya kwa nguvu zote.

0 your comments:

Post a Comment