Afrika Kusini, wenyeji wa michuano ya Kombe la
Mataifa ya Afrika mwaka 2013, imefuzu kucheza hatua ya robo fainali
baada ya kutoka sare ya 2-2 na Morocco.
Kwa matokeo hayo Afrika Kusini inaongoza kundi A ikiwa na pointi 5 sawa na Cape Verde, lakini ikiizidi kwa wingi wa magoli.Matokeo hayo yaliyodumu hadi mapumziko.
Huku Morocco ikiamini kuwa imeshinda, ilishtukia Afrika Kusini wanasawazisha katika dakika ya 71 kupitia kwa Mahlangu.
Morocco haikukata tamaa kusaka ushindi, na iliwezakutia kimiani goli la pili katika dakika ya 82, mfungaji akiwa Abdelilah Elhafidi.
WACHEZAJI WA MOROCCO WAKITOKA NJE YA UWANJA VICHWA CHINI MARA BAADA YA MCHEZO WAO NA WENYEJI AFRIKA KUSINI
Morocco yenye pointi 3 na Angola yenye pointi 1 kutoka kundi A, zimeiaga michuano hiyo ya Kombe la Mataifa ya Afrika ya mwaka 2013.
Kundi B leo litakuwa linakamilisha michezo yake, kwa Ghana kumenyana na Niger, huku DR Congo ikipepetana na Mali.Mpaka sasa Ghana ndiyo inayoongoza kundi hilo ikiwa na pointi 4, ikifuatiwa na Mali pointi 3, DR Congo pointi 2 na Niger imeweka kibindoni pointi 1.
HIVI NDIVYO WENYEJI WA MICHUANO YA AFCON AFRIKA KUSINI WALIVYOSHANGILIA KUFUZU HATUA YA ROBO FAINALI WAKIUNGANA NA CAPE VERDE KATIKA KUNDI LAO.
0 your comments:
Post a Comment