Taarifa kutoka Harare nchini Zimbabwe zinasema jeshi la Polisi nchini humo kituo cha Muchakata limemkamata mwanaume mmoja anayefahamika kwa jina la Emily Mkwende (32) pichani,kwa kosa la kuibaka maiti ya mwanamke aliyetambulika kwa jina la Tineyi Chigedhe(26).
Mwanaume huyo ambaye alikuwa mfanya kazi wa ndani alijisalimisha kituo cha Polisi kijiji cha Nyoka tukio ambalo lilitokea jumatano ya wiki iliyopita na mtu huyo amekuwa akitafutwa na jeshi la polisi lakini ameona ni vema kujisalimisha.Emily alikuwa mfanyakazi wa kazi za ndani na marehemu katika jumba la kifalme la mfalme wa kijiji cha Nyoka anayefahamika kwa jina la mfalme Chiwundura.
Chanzo cha taarifa hii kinasema mwanaume huyo alikuwa akimtaka kimapenzi mfanyakazi mwenzake wa kike(Tineyi) kwa muda mrefu bila mafanikio hatimaye aliamua kutumia nguvu kumwingilia kimwili kwa kumwangusha chini na marehemu kuangukia tumbo kitendo ambacho kilipelekea mwanamke huyo kufariki.
Baada ya Emily kuona mwanamke huyo katulia alichukua uamuzi wa kumwagia ndoo moja ya maji lakini marehemu(Tineyi) hakuweza kuzinduka,kuona hivyo mwanaume huyo akaamua kumalizia adhima yake kwa kuitoa nguo maiti hiyo na kuanza kuibaka.
Msemaji wa Polisi wa kituo hicho Assistant Inspector Emmanuel Mahoko alisema taarifa zaidi hazitatolewa na jeshi la Polisi kwani bado uchunguzi unaendelea chochote kitakachofahamika juu ya tukio hilo umma utafahamishwa"I can confirm that police have arrested a man who is employed as a
domestic worker after he allegedly killed a fellow female workmate
before he later rapèd the corpse. I am not in the office to give finer
details into the matter,".
Lakini chanzo cha habari hii kimesema siku ya tukio Emily Mkwende na Tineyi Chigedhe mida ya usiku waliachwa peke yao na wafanyakazi wenzao waliondoka kwenda sehemu zingine za majukumu na ndipo mtuhumiwa(Emily)alipomtongoza kwa mara nyingine marehemu na ombi lake lilipokataliwa ndipo akaamua kufanya kitendo hicho baada ya kufanya hivyo mtuhumiwa alikimbia, masaa mawili wafanyakazi wenzake na marehemu waliporudi waliikuta maiti ikiwa uchi huku sehemu za siri zikiwa na majimaji ya mbegu za kiume(semen)ndipo taratibu za kuipima maiti kitaalam zikafuata na ikagundulika imebakwa huku ikiwa haiko hai.
Mkwende amekiri makosa na kuongeza kuwa alishawahi kufanya tukio kama hilo huko nyuma,mpaka sasa yupo mahabusu akisubiri kusomewa mashtaka na hukumu yake itakapotolewa na mahakama kwa mujibu wa sheria za Zimbabwe.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 your comments:
Post a Comment