Sheria za soka za sasa zinakataza mawasiliano yoyote ya kieletroniki kati ya wachezaji na makocha na watu wanaohusika na mambo ya afya, lakini kumekuwepo na wito kuibadili sheria hiyo ili kuleta utaratibu wa kuweka vifaa vitakvyokuwa vinafuatilia maendeleo ya afya za wachezaji uwanjani, hasa kufuatiwa kutokea kwa matukio hivi karibuni ya wachezaji kama akina Fabrice Muamba, aliyendondoka uwanjani kufuatiwa kupata mshtuko wa moyo na hatimaye ikabidi aastafu soka
Tukio hili lilishawahi kumkuta pia aliyekuwa kiungo wa kimataifa wa Cameroon Marc Vivien Foe aliyekutana na tatizo kama la Mwamba wakati timu yake ya Taifa ilipokuwa ikimenyana na Colombia katika dimba la Stade de Gerland mjini Lyon, nchini Ufaransa ambapo dakika ya 72 kipindi cha pili na alikimbizwa Hospitalini ambapo tayari alikuwa amefariki
Marc Vivien Foe akiwa hajitambui baada ya kupoteza fahamu |
0 your comments:
Post a Comment