Leo kupitia kipindi cha Jahazi toka Clouds Fm Msanii kutoka Nigeria Martins Okey Justice a.k.a Jmartins aliweza kufunguka juu ya baadhi ya maswali yaliyoelekezwa kwake na Watangazaji wa Kipindi hicho Mussa Hussein,Emmanuel Lekudah naye Wasiwasi Mwabulambo ambaye alikuwa Online tokea Dodoma katika harakati za Tamasha kubwa la Fiesta litakalofanyika mkoani Dodoma hapo kesho.
Kikubwa ambacho Mlelekwa INC ilikifurahia ni jinsi ambavyo Jmartins aliposema anaifahamu vizuri Bongo Flavour kwa sababu yapata miaka 6 sasa yuko kwenye urafiki na AY jambo ambalo lilifanya yeye kuifahamu vizuri Bongo Flavour,Kingine ambacho pia alizungumzia ni namna ambavyo atashirikiana na wasanii wengine tofauti na Ommy Dimpoz,AY MwanaFA kikubwa kama anajua anachokifanya haijalishi majina,alipokuwa akijibu swali lililoelekezwa kwake
CLIP NZIMA YA INTERVIEW HIYO HII HAPA UNAWEZA KUISIKILIZA KAMA HAUKUPATA KUISIKIA.
Sep 12, 2013
Tagged under: Entertainment, Music, News, Social
Hot News | Jmartins aisifia Bongo Flavour ndani ya Jahazi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

0 your comments:
Post a Comment