Hatimae yale
mashindano ya utangazaji katika chuo cha
uandishi wa habari na
utangazaji arusha A.J.T.C yaanza kutimua vumbi leo
utangazaji arusha A.J.T.C yaanza kutimua vumbi leo
Chuo cha
uandishi wa habari na utangazaji arusha
leo kimezinduwa rasmi mashindano ya utangazaji wa vipind mbalimbali vya redio katika studio za radio chuoni hapo
Mashindano
hayo ambayo yanahusisha vipindi mbalimbali vya redio vya usomji wa habari,
matangazo ya vifo, vipindi maalumu na michezo yameanza kwa wakufunzi wa chuo
hicho kuendesha vipindi mbalimbali.
Kipindi cha
kwanza kilikuwa cha DJ Elfuraha samboto
alie endesha kipindi cha muziki mchanganyiko baada ya hapo wakaingia
wasomaji wa habari madam Jackline joel pamoja na madam kagiye kikafuata
kipindi cha michezo safari hii akirejea tena Elfuraha samboto
Mkuu wa idara
ya utangazaji chuoni hapo bwana Onesmo elia mbise aliingia katika kipindi cha
dira ya maisha, kisha kikaendelea kipindi cha matukio kilicho endeshwa na Lukas
modah baada ya matukio bwana Elhuruma chao aliwaburudisha wasikilizaji kwa
kipindi chake cha Gospal Time, Baada ya hapo wasikilizaji wakapata fursa ya
kujuwa wasiyo yajuwa kutoka kwake madam happynes Gaudens na kipindi chake cha
Usiyo yajuwa .
Baada ya
utangulizi huo wa wakufunzi kumaliza
vipidi vyao ndipo lile shindano likaanza rasmi kwa darasa la mount Evarist
kufunguwa dimba na kufanya vipindi vya Habari, matangazo ya vifo habari za
michezo pamoja na kipindi maalum
Mashindano hayo ambayo yanashirikisha madarasa
ya 11 huku 4 yakitokea katika ngazi ya stashahada na
madarasa 7 yakitokea ngazi ya
Astashahada yanatarajiwa
kuendeshwa kwa siku tano kuazia
leo tarehe 21-27/2014 siku ya ijumaa
Bingwa wa mashindano hayo anatarajiwa kuibuka na
kitita cha elfu 60 na kikombe chenye thamani ya shilingi laki moja huku kila mtu binafsi atakae ingia studio
kuliwakilisha darasa lake akipata zawadi.
0 your comments:
Post a Comment